Alikiba na Seven hawawezi kunilipa- Barakah,

October 2, 2020

Msanii Barakah The Prince amemaliza utata uliokuwepo kati yake na msanii Alikiba na meneja Seven Mosha kwa kusema amewasamehe bure kwani hawawezi kumlipa kwa dhuluma walizomfanyia.

Barakah The Prince amesema ameamua kusamehe, kusahau na kutofuatilia yaliyotokea japo anaamini waajiri wake wa zamani bado wana kinyongo naye.

“Naomba leo tufunge mjadala wa Alikiba na Seven Mosha, sina noma na mtu yeyote labda wao ndiyo wana noma na mimi nimezika na nimefukia muda mrefu sana maana hawawezi kuwa na pesa ya kunilipa kwenye kipaji changu kama nikiamua kufuatilia kutokana na dhuluma na vitu vyote walionifanyia, nitakuwa namuonea tu” amesema Barakah The Prince 

Barakah The Prince alisainiwa Rockstar4000 mwaka 2016 chini ya Mkurugenzi na meneja lebo hiyo Seven Mosha na msanii Alikiba ambaye ni mshirika wa kampuni hiyo kwa upande Afrika Mashariki.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *