Aliekuwa Rais wa Mali apelekwa nje ya nchi kwa matibabu, on September 7, 2020 at 10:00 am

September 7, 2020

Rais aliyepinduliwa nchini Mali, Ibrahim Boubacar Keita, amesafirishwa kupelekwa Umoja wa Falme za Kiarabu kwa ajili ya matibabu.Mwanadiplomasia mmoja ambaye hakutaka kutambulishwa jina lakini anafahamu tukio hilo, amesema hayo na kuongeza kwamba Keita ameondoka akiwa pamoja na Mke wake, Madaktari wawili, Mawakala wanne wa kiusalama na msaidizi.Jumanne ya wiki hii Keita alipelekwa katika hospitali moja mjini Bamako na kulazwa ambapo hadi siku ya Alhamisi aliporuhusiwa kutoka hospitalini hapo kwa madai kwamba hali yake ya afya ilikuwa inaendelea vizuri.,

Rais aliyepinduliwa nchini Mali, Ibrahim Boubacar Keita, amesafirishwa kupelekwa Umoja wa Falme za Kiarabu kwa ajili ya matibabu.

Mwanadiplomasia mmoja ambaye hakutaka kutambulishwa jina lakini anafahamu tukio hilo, amesema hayo na kuongeza kwamba Keita ameondoka akiwa pamoja na Mke wake, Madaktari wawili, Mawakala wanne wa kiusalama na msaidizi.

Jumanne ya wiki hii Keita alipelekwa katika hospitali moja mjini Bamako na kulazwa ambapo hadi siku ya Alhamisi aliporuhusiwa kutoka hospitalini hapo kwa madai kwamba hali yake ya afya ilikuwa inaendelea vizuri.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *