Akamatwa mbele ya bunge la Uganda akiwa na kichwa cha mtoto, on September 14, 2020 at 5:00 pm

September 14, 2020

Polisi nchini Uganda imemkamata mbele ya bunge la taifa hilo mwanaume mmoja aliyekuwa amebeba kikapu kilichokuwa na kichwa cha mtoto.Hata hivyo haijawa wazi ni ujumbe gani aliotaka kuufikisha kwa wabunge.Haijafahamika piani wapi na ni kwa vipi alipata kichwa hicho.Kwa sasa mwanaume huyo anashikiliwa katika idara ya upelekezi wa makosa ya jinai , ambako anahojiwa.Chanzo cha habari katika Idara ya upelelezi nchini humo kimesema kwamba kisa cha kutoweka kwa mtoto kiliripotiwa katika wilaya ya Masaka, kusini mwa Kampala, siku ya Jumapili. Mwili wa mtoto ambao haukuwa na kichwa pia ulipatikana siku hiyo hiyo wilayani humo.Wachunguzi wanataka kubaini iwapo tukio hilo lina uhusiano na kichwa ambacho mwanaume huyo amekamatwa nacho.Katika miaka ya 90 hadi mapema 2000 na zaidi, Uganda ilishuhudia wimbi la utekaji nyara na mauaji ya watoto, ambapo iliaminiwa kuwa miili yao ilitumiwa kama kafara.Na katika miaka ya hivi karibuni, kumekuwa na matukio ya wananaharakati wanaotupa vitoto vya nguruwe katika maeneo ya bunge, kama ishara ya kupinga ufisadi na ukosefu wa ajira kwa vijana.,

Polisi nchini Uganda imemkamata mbele ya bunge la taifa hilo mwanaume mmoja aliyekuwa amebeba kikapu kilichokuwa na kichwa cha mtoto.

Hata hivyo haijawa wazi ni ujumbe gani aliotaka kuufikisha kwa wabunge.

Haijafahamika piani wapi na ni kwa vipi alipata kichwa hicho.

Kwa sasa mwanaume huyo anashikiliwa katika idara ya upelekezi wa makosa ya jinai , ambako anahojiwa.

Chanzo cha habari katika Idara ya upelelezi nchini humo kimesema kwamba kisa cha kutoweka kwa mtoto kiliripotiwa katika wilaya ya Masaka, kusini mwa Kampala, siku ya Jumapili. Mwili wa mtoto ambao haukuwa na kichwa pia ulipatikana siku hiyo hiyo wilayani humo.

Wachunguzi wanataka kubaini iwapo tukio hilo lina uhusiano na kichwa ambacho mwanaume huyo amekamatwa nacho.

Katika miaka ya 90 hadi mapema 2000 na zaidi, Uganda ilishuhudia wimbi la utekaji nyara na mauaji ya watoto, ambapo iliaminiwa kuwa miili yao ilitumiwa kama kafara.

Na katika miaka ya hivi karibuni, kumekuwa na matukio ya wananaharakati wanaotupa vitoto vya nguruwe katika maeneo ya bunge, kama ishara ya kupinga ufisadi na ukosefu wa ajira kwa vijana.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *