Ajali ya mgodini yauwa wachimbaji 19 nchini Pakistan, on September 8, 2020 at 3:00 pm

September 8, 2020

Watu wasiopungua 19 wameuawa baada ya kuangukiwa na kipande cha mwamba katika machimbo ya marumaru kaskazini magharibi mwa Pakistani.Maafisa nchini humo wanasema bado shughuli za uokozi zinaendelea kutafuta miili ya watu wengine iliyonaswa chini ya udongo. Tariq Habib ambaye ni afisa mkuu wa polisi katika wilaya ya Khyber-Pakhtunkhwa, amesema kipande kikubwa cha mwamba kimewaangukia wachimbaji usiku wa kuamkia leo, na kuongeza kuwa hadi asubuhi miili saba ilikuwa imekwishapatikana.Kiongozi wa eneo ulipo mgodi huo Iftikhar Ahmed amesema watu kati ya 20 na 25 walikuwemo ndani ya mgodi huo ajali ilipotokea, na kuelezea hofu kuwa idadi ya waliouawa inaweza kupanda.Polisi imesema mwamba uliowaangukia wachimba migodi umeziba pia lango la kutokea mgodini, na kuwazuia kutoka waliokuwa bado hai kwa saa takribani saba. Mamia ya wachimbaji wa madini huuawa kila mwaka nchini Pakistan kutokana na mazingira duni ya utendaji kazi.,

Watu wasiopungua 19 wameuawa baada ya kuangukiwa na kipande cha mwamba katika machimbo ya marumaru kaskazini magharibi mwa Pakistani.

Maafisa nchini humo wanasema bado shughuli za uokozi zinaendelea kutafuta miili ya watu wengine iliyonaswa chini ya udongo. Tariq Habib ambaye ni afisa mkuu wa polisi katika wilaya ya Khyber-Pakhtunkhwa, amesema kipande kikubwa cha mwamba kimewaangukia wachimbaji usiku wa kuamkia leo, na kuongeza kuwa hadi asubuhi miili saba ilikuwa imekwishapatikana.

Kiongozi wa eneo ulipo mgodi huo Iftikhar Ahmed amesema watu kati ya 20 na 25 walikuwemo ndani ya mgodi huo ajali ilipotokea, na kuelezea hofu kuwa idadi ya waliouawa inaweza kupanda.

Polisi imesema mwamba uliowaangukia wachimba migodi umeziba pia lango la kutokea mgodini, na kuwazuia kutoka waliokuwa bado hai kwa saa takribani saba. Mamia ya wachimbaji wa madini huuawa kila mwaka nchini Pakistan kutokana na mazingira duni ya utendaji kazi.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *