Agri Thamani yaingia makubaliano na Word Vegetable Center kutokomeza utapiamlo na udumavu hapa nchini,

October 6, 2020

 

Taasisi isiyo ya kiserikali ya Agri Thamani imesaini makubaliano ya kushirikiana na World Vegetable Centre, Shirika la Kimaitaifa linalofanya kazi kwenye nchi 25 za Afrika ambao ni Wabobezi kwenye Masuala ya Mbegu za Mboga Mboga ili kutoa elimu ya Kilimo na lishe mashuleni na Jamii kwa ujumla..

Mkataba huo wa Kushirikiana umetiwa saini na mkurugenzi wa taasisi ya Agri Thamani bi Neema Lugangira na mkurugenzi wa Africa mashariki na kusini wa kitu cha utafiti cha Mbogamboga na matunda cha kimataifa cha (World Vegetable Center) Dr. Gabriel Rugalema tarehe 5 Oktoba 2020, Jijini Arusha zoezi ambalo liliambatana na Taasisi ya Agri Thamani kupokea packet 500 za Mbegu Bora za MbogaMboga Mchanganyiko zenye Viini Lishe vingi. 

Mkurugenzi wa Taasisi ya Agri Thamanani amesema kuwa packet hizo zitakwenda kutumika kuanzisha Bustani za Mboga Mashuleni, Kaya na Jamii kwa ujumla ambapo ametaja maeneo mkuu ya mkataba huo ni 1. Kueneza Elimu ya Kilimo na Lishe Mashuleni na Jamii, 2. Kuweka msukumo na kuhamasisha ulaji wa mbogamboga na matunda, 3. Kuanzisha bustani za mbogamboga mashuleni, kaya na bustani za mfano kwenye jamii, 4. Kuwafikia, kuwajengea uelewa na kuwahamasisha Waandishi wa Habari, Viongozi wa Dini, Viongozi wa Kisiasa, Mama Lishe kama Wadau Muhimu kusaidia kueneza Elimu ya Lishe na Umuhimu wa Uzalishaji na Ulaji wa MbogaMboga na Matunda na Lishe, 5. Kuangazia sana wanawake na vijana kushiriki katika mnyororo wa thamani wa mazao ya MbogaMboga, Matunda na Lishe, 6. Kusaidia kwenye kutunga Sera na Mipango Kazi rafiki kwa Tasnia ya Kilimo cha MbogaMboga, Matunda na Lishe.

Aidha, amesema kuwa utekelezaji huo utaanzia kwenye Mikoa 6 ambayo ni Kagera, Dodoma, Tabora, Tanga, Kigoma na Geita.

Bi, Neema amemuhakikishia Dr. Gabriel Rugalema kuwa kupitia makubaliano haya na kwa kushirikiana na Serikali na Wadau wengine wataimarisha Uzalishaji na Ulaji wa MbogaMboga na Matunda hali ambayo itapelekea kutokomeza Udumavu na Utapiamlo kwa ujumla nchini Tanzania.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *