Afisa wa polisi aliyemuua mtu mweusi afutwa kazi Marekani

October 11, 2020

 

Shaun Lucas, ambaye ni afisa wa polisi aliyehusika na muaji ya mchezaji wa zamani wa American Football Jonathan Price kutumia silaha ya umeme katika jimbo la Texas, ameripotiwa kuachishwa kazi.

Katika maelezo yaliyotolewa na utawala wa Wolfe City, iliarifiwa kuwa afisa huyo katili Lucas mwenye umri wa miaka 22 alifutwa kazi kutokana na mauji hayo.

Maelezo zaidi yanaarifu kuwa utawala wa mji ulimchukulia Lucas hatua hiyo kwa kuzingatia kosa la ‘‘ukiukaji mkubwa’’ wa kanuni za idara ya polisi.

Wakili wa Price, Lee Merritt, alifahamisha kuwa familia yake iliridhishwa na taarifa hizo za kufutwa kazi kwa Lucas, ingawa walitarajia uamuzi huo kuchukuliwa tangu mwanzoni.

Usiku wa Jumamosi baada ya polisi kupewa taarifa za kuzukwa kwa ugomvi nje ya duka moja la ununuzi, Lucas alielekea kwenye eneo la tukio na kutaka kumkamata Price ambaye ni Mmarekani mwenye asili ya Kiafrika.

Price mwenye umri wa miaka 31 alinyanyua mikono hewani na kutaka kujisogeza mbali na polisi. Lucas akamkabili kwa kutumia silaha ya umeme na baadaye akamuua kwa kumpiga risasi.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *