Afisa aliyehusika na mauaji ya Floyd aachiliwa huru kwa dhamana,

October 9, 2020

 Mahakama ya Minnesota imetangaza kumwachiliwa huru Chauvin ambaye ni mmoja wa  maafisa waliohusika na mauaji ya George Floyd.

Chauvin ambaye alikuwa akizuiwa katika gereza la Oak Park Heights tangu mwezi Mei, aliachiliwa huru baada ya kulipa dhamana ya fedha dola milioni 1 iliyoidhaminiwa na shirika la ”Allegheny Casualty Company.

Hapo awali, maafisa wa polisi 3 kati ya 4 waliokutwa na hatia kufuatia kifo cha Floyd, pia waliwahi kuachiliwa kwa dhamana ya fedha dola 750,000.

Baada ya  Derek Chauvin kuachiliwa, sasa maafisa wote walioshtakiwa kwa mauaji ya Floyd wamekuwa huru.

Hata hivyo Chauvin na maafisa wengine 3 wa polisi wanaokabiliwa na kesi ya mauaji ya daraja la pili, wanatarajiwa kusimamishwa kizimbani mwezi Machi mwaka 2021.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *