Afghanistan yaishutumu Taliban kwa kuvuruga amani nchini,

October 11, 2020

 Serikali ya Afghanistan imelishutumu kundi la Taliban kwa kutoa visingizio kuhusu mchakato wa amani na kuendeleza vurugu.

Makamu wa rais wa Afghanistan Sarwar Danish, alihutubia hafla moja aliyohudhuria katika mji mkuu wa Kabul na kusema kuwa Taliban haina sababu yoyote ya kupigana na serikali ya nchi.

Akielezea Taliban kuendeleza harakati zao za kuvuruga amani mjini Kabul hivi karibuni, Danish alisema, ‘‘serikali ya Afghanistan imekuwa mstari wa mbele muda wote ili kudumisha amani nchini, ilhali Taliban imekuwa ikivuruga kwa visingizio.’’

Marekani ilianzisha mazungumzo ya kupunguza vurugu na Taliban mnamo mwezi Desemba 2019, na kuishia kwa makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyotiwa saini tarehe 29 Februari.

Kufuatia hatua hiyo, mchakato wa mazungumzo kati ya kundi la Taliban na serikali ya Afghanistan ukaanzishwa tarehe 12 Septemba katika mji mkuu wa Doha nchini Qatar.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *