October 13, 2020

MSHAMBULIAJI wa zamani wa Simba, Mrundi, Laudit Mavugo amefunguka kuwa Yanga ina bahati kubwa ya kuweza kumnasa kocha Cedric Kaze kwa kuwa anaamini sasa wanaweza kucheza soka la pasi katika uwanja wowote wataokwenda kucheza kutokana na kocha huyo kuwa na utalaam huo.

Mavugo ametoa kauli hiyo kufuatia uongozi wa Yanga kumalizana na Kaze ambaye anakuja kubeba mikoba ya Mserbia, Zlatko Krmpotic, aliyesitishiwa kibarua chake.

Kaze alitarajia kuingia Afrika Mashariki pamoja na mazingira ya viwanja vyake. “Unajua shida ya nchi zetu zipo kwenye viwanja ambavyo vingi vimekosa ubora wa kutosha lakini bado naamini Yanga wataona faida ya kuwa na Kaze kwa sababu timu itaweza kucheza soka la kuvutia kwa pasi nyingi katika uwanja wowote ambao watakwenda nchini Jumamosi iliyopita kabla ya kubadilisha ratiba yake na sasa anatarajia kuwasili nchini Alhamisi ya wiki hii, tayari kwa kuanza majukumu yake ndani ya timu hiyo.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Mavugo alisema kuwa Yanga wataona faida ya kuwa na kocha mwenyewe uelewa mkubwa na soka la kucheza.

“Uzuri nimecheza hapo na naelewa lakini nimefanya kazi na kocha Kaze wakati nilipokuwa Atletico, naongea kitu ambacho nakijua juu yake lakini yeye mwenyewe siyo mgeni na mazingira ya Tanzania pamoja na mpira wake, hivyo mashabiki wa Yanga watarajie makubwa kutoka kwake,” alisema Mavugo.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *